Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame, ameunga mkono kufungwa kwa takribani makanisa 8,000 ambayo ukaguzi huo ulibaini kuwa hayafuati sheria, akiwaonya wajasiriamali wanaolenga kuwaibia Wanyarwanda mali zao, wakitanguriza mbere jina la Mungu.
Kauri hii Raisi Kagame ameitowa baada ya kupokea viapo vya Wabunge 80 hiileo tarehe 15 Agosti 2024
Rais Kagame amesema
kabla ya kuhoji kuhusu kufungwa kwa makanisa , watu wahoji jinsi yalivyoanzishwa.
Alisema, “Maana ya makanisa ni nini? Mara ya kwanza mlipiga kelele, 'Wamefunga makanisa'. Hapo mwanzo mlianza kusema 'imeendaje?' Maelfu ya makanisa ni nini? Wanyarwanda mna shida gani? Lakini nadhani ni suala la kuwa Mwafrika. Sisi Waafrika tuna tatizo kweli kweli.”
Mkuu huyo wa nchi amesema kuwa makanisa hayo lazima yatimize matakwa yaliyowekwa na sheria. wale ambao hawatazingatia sheria makanisa yao yatafungwa.
Alisema, “Kile ambacho hakitii sheria, hakipaswi kutokea. Hapo ndipo nilipowaona wakisema, ‘Kwanza Rais hajui Jambo la kufunga makanisa eti ni dhambi.' sitaki. Hakika nitapambana nayo.”
Amewataka wabunge hao kuungana na taasisi nyingine kuweka mfumo unaowaongoza Wanyarwanda katika njia sahihi, na kwamba ma Pasita wenye lengo la kuwaibia wananchi mali chache walizonazo, ni dhahiri wakomeshwe.
Bagabo John