Waziri wa Serikali za Mitaa, Musabyimana Jean Claude, ametangaza kuwa ukaguzi uliofanyika kwenye nyumba za ibada yaani mahekalu, misikiti na makanisa ulisababisha kufungwa kwa nyumba 9880 za ibada.
Katika mahojiano na na vyombo vya Habari wiki hii mnamo Septemba 1, 2024.
Waziri Musabyimana ameeleza kuwa ukaguzi huo ulifanyika kutokana na ongezeko la mashirika ya kidini na kimila hali iliyopelekea maeneo mengi ya ibada kutokidhi matakwa.
Alifahamisha kuwa katika ukaguzi huo ilibainika kuwa nchini Rwanda kuna dini, makanisa na mashirika 563 yenye misingi ya imani zikiwemo 345 za dini mbalimbali.
Alisisitiza kuwa ongezeko lake si muhimu bali wengi wameendeleza mafundisho potofu na wengine wanafanya kazi katika maeneo ambayo hayakidhi matakwa.
Alisema, “Kuna mafundisho yanayoleta matatizo, unabii unaotisha watu, unawahimiza kuasi mipango ya serikali, kupanda migawanyiko. Jambo lingine ambalo tumekuwa tukiliona ni kutokana na ongezeko la dini ambalo limepelekea kufunguliwa kwa maeneo ya ibada yasiyokidhi matakwa ambayo yangefanya mahali hapo kuwakaribisha watu.
Wakati wa ukaguzi huo, iligunduliwa kwamba kulikuwa na maeneo mengine ya ibada yapatayo 110 nje ya hekalu ambayo yalifungwa mara moja
Ukaguzi huo pia ulipelekea kufungwa kwa misikiti isiyofuata sheria ambapo ni asilimia 29.89 tu ya misikiti yote iliyokaguliwa ndiyo inayofanya kazi kwa sasa.
Alisema, “Tulikagua makanisa au nyumba za ibada 14,093 kote nchini, na kubaini kuwa nyumba 9,880 kati ya hizo hazikidhi mahitaji ya ibada, ambayo ni 70,1%
Alisema, kwa mfano, kuna sehemu kuna chumba cha harusi, baa au sehemu ya burudani, lakini unakuta Jumapili kuna mhubiri anakodisha na kuwaita Wakristo waje kusali hapo.
Waziri wa Serikali za Mitaa Musabyimana Jean Claude
Waziri Musabyimana pia alisema mbali na nyumba za ibada kufungwa, kuna Mashirika na dini 47 ambazo zimenyimwa haki ya kufanya kazi nchini Rwanda.
Hii inatokana na ukweli kwamba wengine hawakuwa na hati zinazo waruhusu kufanya kazi nchini Rwanda.
Bagabo John