•     

Rwanda: Wanajeshi zaidi ya 1100 wamestaafishwa

Jenerali Jean Bosco Kazura ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Jashi la Rwanda ni mmoja wa wanajeshi 1,167 waliostaafishwa.

Wanajeshi zaidi ya 1100 wamestaafishwa

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Rwanda, inasema kuwa Rais Kagame na Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Rwanda, amethibitisha kuwa wanajeshi hao akiwemo Jenerali Jean Bosco Kazura na wengine wanne wenye cheo cha Brigedia Jenerali wamestaafishwa.

Hao ni Brig Jenerali John Bagabo, Brig Jenerali John Bosco Rutikanga, Brig Jenerali Johnson Hodari na Brig Jenerali Firmin Bayingana.

Mkuu huyo wa nchi pia amethibitisha kuwa maafisa wengine wakuu 170 na askari wengine 992 wa vyeo mbalimbali wanakwenda likizo.

Jenerali Kazura amekuwa katika uongozi wa Jeshi la Rwanda kwa miaka mingi kwani kuanzia Novemba 2019 hadi Juni 2023 alikuwa Mkuu wa Majeshi.

Pia amewahi kushika nyadhifa nyingine mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Kijeshi cha Nyakinama.

Katika hafla ya kuwaaga askari hao, Waziri wa Ulinzi, Juvenal Marizamunda, amewashukuru kwa mchango wao katika maendeleo ya Rwanda tangu ukombozi wa nchi hiyo, kusitisha mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na safari ya maendeleo ambayo nchi hiyo ipo hivi sasa.

           Jeneral Mstaafu Kazura Jean Bosco 

Mkuu wa Majeshi ya Rwanda, Jenerali Mubarakh Mukanga, amesema kila hatua wanayopiga ni pamoja na kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza wajibu wao wa kulinda nchi.

Alisema, "Mliitumikia nchi yetu kwa kujitolea, mtajivunia mchango wenu kwa amani na usalama wetu., sio tu kutimiza majukumu yako, lakini pia kuifanya RDF kuwa Jeshi linaloheshimika."

Bagabo John