•     

Aziz Ki hatashiriki katika Mchezo wa hatua ya 16 bora

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Burkina Faso, Stéphane Aziz Ki hatashiriki katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano ya AFCON dhidi ya Ivory Coast unaopigwa leo.

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Burkina Faso limeidhinisha mchezaji huyo kuondoka kambini ili akajiunge na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

​Sababu ya kuondoka kwa nyota huyo ni kufuatia kifo cha ndugu yake wa karibu, ambaye ni mpwa wake, lakini Aziz Ki alikuwa akimchukulia na kumpenda kama mwanawe wa kumzaa. Taarifa hizi zimeleta simanzi kubwa kwa kikosi cha "The Stallions" na wadau wa soka barani Afrika ambao walikuwa wakitarajia kuona ufundi wake uwanjani leo.

​Pigo hili linakuja wakati mchezaji huyo akiwa katika kiwango bora tangu ajiunge na klabu yake ya Wydad Casablanca.

Bagabo John 