Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba, ameipongeza kwa dhati Timu ya Taifa, Taifa Stars, kwa kiwango walichokionesha katika mashindano ya AFCON nchini Morocco.
Amesema kuwa ingawa timu hiyo imeyaaga mashindano, haikutoka bali "imetolewa" kutokana na mazingira ya mchezo, hasa katika dakika za mwisho za mchezo wao wa mwisho.

Kufuatia ushujaa huo, Waziri Mkuu amewaelekeza Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, pamoja na Wizara ya Michezo, kuandaa mapokezi ya kishujaa kwa vijana hao watakaporejea nchini.
