Rais wa Paul Kagame ameipongeza Paris Saint-Germain (PSG) baada ya kutwaa ubingwa wa UEFA Champions League, akieleza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya safari ya kuvutia ambayo timu hiyo imeonyesha katika mashindano hayo. Kagame pia alisifu ushirikiano wa PSG na kampeni ya “Visit Rwanda”, akibainisha kuwa ushindi huo unaendelea kuitangaza Rwanda katika jukwaa la kimataifa kupitia michezo.
Paris Saint-Germain (PSG) ilitwaa ubingwa wa UEFA Champions League baada ya kuifunga Arsenal kwa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1 iliyodumu kwa dakika 120 za mchezo wa fainali uliochezwa katika Uwanja wa Puskás Aréna mjini Budapest, Hungary, jioni ya Jumamosi hii.

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X baada ya mchezo huo, Rais Paul Kagame aliipongeza Paris Saint-Germain (PSG) kwa kutwaa taji la UEFA Champions League la msimu wa 2025/26.
“Hongera kwa mshirika wa Visit Rwanda, Paris Saint-Germain, kwa kutwaa UEFA Champions League, taji ambalo walilistahili na kulinyakua kwa mara ya pili mfululizo,” alisema Rais Kagame.

Pia aliipongeza Arsenal kwa kufika fainali na kupambana hadi dakika ya mwisho ya mchezo. “Hongera pia kwa Arsenal kwa kufika fainali na kupigana hadi dakika za mwisho kabisa.
Timu zote mbili zimewapa fahari mashabiki wao, huku PSG ikionyesha kwa mara nyingine kuwa ni timu bora zaidi,” aliongeza.
Ushindi huo umeiwezesha PSG kutwaa taji la kwanza la Champions League katika historia ya klabu hiyo
Bagabo John
