Uongozi wa Jeshi la Rwanda (RDF) umethibitisha kifo cha Luteni Jenerali Kabandana aliyefariki dunia asubuhi ya Jumapili katika Hospitali ya Kijeshi ya Kanombe, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na RDF, jeshi hilo limeeleza masikitiko yake makubwa na kufikisha salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, likisema linaungana nao katika kipindi hiki kigumu.
Marehemu Lt Gen Kabandana alijiunga na Jeshi la Rwanda mwaka 1990, na alikuwa miongoni mwa wanajeshi waliotoa mchango mkubwa katika ukombozi wa nchi na kusitisha mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994.

Taarifa kuhusu maandalizi ya mazishi na shughuli nyingine zinazohusiana na kuaga mwili wake, zinatarajiwa kutolewa na RDF pamoja na familia yake katika siku zijazo
Bagabo John
