Tanzania imewazuia waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ambazo zote ni jumuiya ambazo nchi hiyo ni mwanachama, kushiriki katika uchaguzi wa Oktoba 29. Badala yake, imezipa vibali balozi 12 za nchi za Magharibi zilizoko nchini kushiriki kama waangalizi.
Uchaguzi wa mwaka huu umevutia uangalizi wa kimataifa zaidi ya kawaida kutokana na kile kinachoonekana kama mgongano na misingi na thamani za kidemokrasia katika maandalizi yake.

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imekosolewa vikali kwa kukandamiza kwa nguvu sauti za upinzani zilizokuwa zikidai mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili kuepusha kurudiwa kwa matukio ya uchaguzi wa mwaka 2020 na chaguzi za serikali za mitaa za mwaka 2019 na 2024, ambazo zote zilighubikwa na madai ya wizi wa kura kwa manufaa ya chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Vyama vyote vingine 19 vilivyosajiliwa nchini Tanzania, mbali na Chadema, vinatarajiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo.
Bagabo John
