Kiongozi wa Chama cha Kijani (DGPR)Democratic Green Party of Rwanda Mh Dkt Frank Habineza, amesema hakuna kitu chochote zaidi ya mazungumzo kinachopaswa kumuingiza mtu yeyote madarakani.
Katika hotuba yake Mhe Dkt Frank Habineza amewakumbusha wanachama mipango na malengo ya chama anachokiongoza na kusisitiza kuwa chama cha Democratic Green Party of Rwanda (Greenparty) hakikubariani mabadiliko ya serikali kwa kutumia nguvu za kijeshi au njia nyingine zinazotishia uhuru wa wananchi
Hapa amesema" Mazungumzo ndiyo njia pekee ya kutatua matatizo,”

Mh Dkt Frank Habineza Mwenyekiti wa Chama cha Upinzani cha Kijani (DGPR)
Aliendelea kusisitiza kuwa chama cha DGPR hakiungi mkono kupinduliwa kwa serikali kwa kutumia silaha, vita na njia nyinginezo zinazotishia uhuru wa watu au kitu chochote kinachoweza kusababisha umwagaji wa damu.

Pia Dkt Habineza amesema chama kinaamini kuwa watu wanapaswa kuzungumza kwa sababu ndiyo njia pekee ya kutatua matatizo.

Katika Mkutano huo urio fanyika hii leo Jumamosi tarehe 10 Mei 2025
Chama hicho kimewachaguwa makamishna wapya na ku idhinishwa.
Bagabo John
