Viongozi wamelaani mashambulizi dhidi ya vikosi vya SADC vilivyotumwa katika kanda hiyo na kuamua kutuma mawaziri wa ulinzi na maafisa wakuu wa kijeshi kushughulikia hali hiyo.
Mkutano huo ulisisitiza kuwarejesha makwao wanajeshi walioshindwa vita, pia na kuwatibu waliojeruhiwa, na kufanya mazungumzo na wadau wote, ikiwa ni pamoja na makundi yenye silaha yasiyo ya serikali, ili kufikia usitishaji mapigano chini ya mchakato wa Luanda na Nairobi.


Hata hivyo, viongozi wakuu, ikiwa ni pamoja na rais wa Angola, hawakuwepo, na kuibua wasiwasi kuhusu umoja wa SADC.
Bagabo John
