•     

Siwezi kukaa kwenye Chama kilichoua watu 29.October- Peter Msigwa

Aliyekuwa kada wa CCM na Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, amezua mjadala mkubwa baada ya kutangaza kurejea ndani ya chama cha upinzani cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akieleza kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kile alichokiita “ukweli na haki” vinavyopatikana ndani ya chama hicho

Msigwa arejea Chadema

Msigwa alisema kuwa tukio lililotokea Oktoba 29, 2025 ndani ya CCM lilimuumiza sana na kumfanya aamini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Katika kauli yake, alidai kuwa yaliyotokea siku hiyo yalikuwa “dhuluma dhidi ya uhai wa binadamu,” jambo lililomfanya kubadili msimamo wake wa kisiasa na kurejea CHADEMA baada ya kuwa ndani ya CCM kwa kipindi kifupi. 

Kauli hiyo imeonekana kuwa ya uzito mkubwa katika siasa za Tanzania, hasa kutokana na historia ya Msigwa ambaye aliwahi kuwa mmoja wa viongozi mashuhuri wa CHADEMA kabla ya kuhamia CCM mwaka 2024.

Wakati huo, alisema alikuwa ameondoka CHADEMA kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa ndani wa chama hicho.

Kurejea kwake CHADEMA kumechukuliwa na baadhi ya wachambuzi wa siasa kama ishara ya kuendelea kwa mvutano wa kisiasa nchini Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu, huku wengine wakiona hatua hiyo kama jaribio la kurejesha ushawishi wake ndani ya siasa za upinzani.

Mitandaoni, kauli yake imeibua mijadala mikubwa, ambapo baadhi ya wananchi wamepongeza uamuzi wake huku wengine wakimtuhumu kubadili misimamo ya kisiasa mara kwa mara.

Bagabo John