•     

Makonda kwenda Morocco kupokea Kijiti Cha Afcon

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo Paul Makonda amesema ameagizwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenda nchini Morocco kwaajili ya kupokea kijiti cha maandalizi ya mashindano ya Afcon 2025.

Makonda kwenda Morocco Kupokea Kijiti Cha Afcon

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 16 Mhe.Makonda amesisitiza kuwa Rais wa Tanzania anataka mashindano ya mwaka 2027 ya Afcon yawe makubwa na ya mfano katika nchi ya Tanzania.

‘’Baada ya kuhitimisha mashindano yaliyopo na kupewa nafasi ya kukabidhiwa na kuanza maandalizi ya michuano ya 2027 kama ambavyo watanzania wengi mnafahamu, Mheshimiwa  Samia amedhamiria kwa dhati na kwa nguvu zake zote kuiweka ramani ya Tanzania kwenye ramani ya dunia kwenye michezo’’ amesema Makonda

Aidha Makonda amesisitiza baada tu ya kukabidhiwa kijiti cha mashindano hayo ni rasmi kampeni za mashindano hayo itaanza kwa haraka na kwa ukubwa wake.

Bagabo John 