•     

Mkutano wa Kimataifa wa Vijana Wajadili Masuala ya Mazingira, Demokrasia na Usawa wa Kijinsia

Vijana kutoka nchi za Kenya, Rwanda na Denmark wamekutana katika mkutano wa kimataifa kujadili masuala muhimu yanayohusu kulinda mazingira, kuendeleza demokrasia jumuishi, na kukuza amani na usawa wa kijinsia katika ngazi ya kimataifa.

Kwa upande wa vijana kutoka chama cha Democratic Green Party of Rwanda, wamesisitiza kuwa mada hizi ni za msingi na ni wajibu wao kuendelea kuzitetea na kuzifanyia kazi kwa nguvu zote, hasa kwa kuwa ndizo nguzo kuu za maendeleo endelevu na haki kwa vizazi vijavyo.

Katika mkutano huo, ujulikanao kama International Eco-Socialism Youth Summit, uliolenga kujadili uchumi unaojali mazingira na kuhimiza haki kijamii, Neto Agostinhn ambaye ni kiongozi kutoka chama cha United Green Movement nchini Kenya, alieleza kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana ni tishio kubwa kwa mustakabali wa nchi yake.

Katika hotuba yake, Agostinhn alitaja kuwa ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana unasababishwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kasoro katika mifumo ya elimu, maendeleo hafifu ya mafunzo ya kiufundi, na ukosefu wa fursa za ujasiriamali kwa vijana.

Kwa ujumla, mkutano huu umewapa vijana jukwaa muhimu la kubadilishana mawazo na mikakati ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao, huku wakitambua kuwa wao ndio nguzo kuu ya mabadiliko ya kweli katika dunia ya leo.

Bagabo John