•     

Polisi wanaojiandaa kwenda katika ujumbe wa amani wamepewa ushauri

Naibu Mkuu wa Polisi wa Rwanda anayeshughulikia operesheni (DIGP), CP Vincent Sano, Jumanne tarehe 10 Machi, aliwataka maafisa wa polisi wanaojiandaa kwenda katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) kudumisha nidhamu na kuiletea heshima Rwanda watakayokuwa wakiwakilisha.

Ushauri huo aliutoa kwa maafisa wa polisi 140 wanaounda kikosi cha RWAFPU3-4 kinachoongozwa na Chief Superintendent of Police (CSP) Emmanuel Hitayezu, ambao wanajiandaa kwenda kuchukua nafasi ya wenzao waliomaliza zaidi ya mwaka mmoja katika mji wa Bangassou ulioko kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

DIGP Sano aliwashukuru kwa bidii na kujitolea walikoonyesha wakati wa mafunzo yao, na akawahimiza kuendelea kuzingatia maadili yanayowatambulisha Polisi wa Rwanda, kufanya kazi kwa ushirikiano na kuheshimu tamaduni za wengine watakaokutana nao katika ujumbe wa kulinda amani; wakiona desturi nzuri wazichukue, lakini waepuke kuiga tabia mbaya.

Tangu mwaka 2014, Rwanda ilianza kutuma maafisa wa polisi katika ujumbe wa kulinda amani na usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa lengo la kusaidia kurejesha utulivu na kuimarisha amani ya kudumu, baada ya miaka mingi ya vita na migogoro ya kikabila pamoja na makundi yenye silaha.

Kwa sasa, kuna vikosi vinne vya Polisi wa Rwanda.
vinavyotekeleza majukumu yao katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, ambayo ni Bangui, Bangassou na Kaga Bandoro.

Bagabo John