Rais Kagame amempokea ofisini kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mahamoud Thabit Kombo. Mazungumzo yao yalilenga kuimarisha zaidi uhusiano mzuri uliopo kati ya Rwanda na Tanzania.
Mazungumzo yaliyowakutanisha viongozi hao wawili yalifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Nchi, Village Urugwiro, tarehe 31 Machi 2026.

Taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti ya X ya Village Urugwiro inaeleza kuwa Rais Kagame na Mahamoud Thabit Kombo walifanya mazungumzo yaliyojikita katika kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Rwanda na Tanzania.

Rwanda na Tanzania zina uhusiano imara katika nyanja mbalimbali, zikiwemo ushirikiano katika teknolojia na mawasiliano. Nchi hizi mbili pia zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya usafirishaji wa watu na bidhaa, elimu, pamoja na kanuni zinazosimamia sekta ya dawa.
Bagabo John
