Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema miundombinu ya Mkoa huo imeendelea kudumu na kuimarika kutokana na ufanisi wa vyombo vya ulinzi na usalama, ambavyo vimefanya kazi kubwa katika kudhibiti athari za maandamano ya Oktoba 29, 2025.
Akizungumza leo Novemba 24, 2025 katika mkutano wa Dkt. Mwigulu Nchemba na wananchi wa Jimbo la Kibamba, Chalamila amesema bila juhudi hizo, madhara ya maandamano hayo yangeweza kusababisha hasara kubwa na kuathiri miundombinu mingi zaidi.

Ametoa wito kwa wazazi kuzungumza na watoto wao na kuwaelimisha kuhusu madhara ya kushiriki maandamano yenye uvunjifu wa amani.
"Tugombane tunavyoweza kugombana, lakini kamwe tusiendelee kuichoma nchi yetu wenyewe. Tukilipua nchi hii lazima na sisi tutakufa. Itakuwa ni kufanya fujo kama kukata mti wakati tuko kwenye tawi la mti huo," amesema Chalamila
Bagabo John
