Vikosi vya jeshi na polisi vimezingira nyumba ya mgombea urais wa upinzani Robert Kyagulanyi Ssentamu (anayejulikana kama Bobi Wine) na mkewe, na hivyo kumweka yeye na familia yake chini ya kizuizi cha nyumbani (house arrest) wakati wa uchaguzi mkuu wa leo.
Taarifa kutoka kwa chama chake, National Unity Platform (NUP), zinasema maafisa wa usalama wameingia kwa kuvunja uzio wa nyumba yake na sasa wanaweka hema ndani ya kiwanja chake.
Hii inafanyika siku ya uchaguzi ambapo wagombea wakuu ni Bobi Wine (NUP) na Rais wa sasa Yoweri Museveni (NRM), ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 40.

Wakati huo huo, mtandao wa intaneti umezimwa nchini Uganda, na kuna madai ya upandaji kura kwa wingi (ballot stuffing), kukamatwa kwa maajenti wa NUP, na kufukuzwa kwa wengine kwenye vituo vya kupigia kura. Bobi Wine ametoa wito kwa wananchi "kuinuka na kukataa utawala wa jinai" kupitia chapisho lake kwenye X.
Bagabo John
