•     

Chama cha ATM Kimependekeza kubadili Jina la nchi

Chama cha ATM Kimependekeza kubadiri Jina la nchi ya Afrika kusini na kuitwa "Azania" ikieleza kuwa jina la sasa ni Chapa ya Kikoloni iliyorithiwa kutoka kwa tawala za Waingereza na Makaburu.

Kwa mujibu wa kiongozi wa chama hicho, Vuyo Zungula, lengo la pendekezo hilo ni kurejesha utambulisho wa taifa na kurudisha urithi wa kihistoria wa watu wa Afrika Kusini. Hata hivyo, baadhi ya wakosoaji wakiwemo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa jina “Azania” halina mizizi imara ya kihistoria wala umaarufu mpana wa kiutamaduni ndani ya nchi.

Pendekezo hili ni sehemu ya juhudi za mabadiliko mapana ya kikatiba yanayolenga kulitazama upya jina, maadili na misingi ya kitaifa ya Afrika Kusini.

Kwa mara ya mwisho, Afrika Kusini ilifanya mabadiliko makubwa ya katiba mwaka 1996, ambapo Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Afrika Kusini (Constitution of the Republic of South Africa, 1996) ilipitishwa rasmi. Katiba hiyo ya 1996 ndiyo inayoendelea kutumika hadi leo japo nayo inabadilishwa.

Bagabo John 