•     

Jeshi lililositisha mauaji ya kimbari bado lipo – Waziri Nduhungirehe aonya wanaotaka kuvuruga Rwanda

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano, Balozi Olivier Nduhungirehe, ameonya wanaotaka kuvuruga usalama wa Rwanda kwamba jeshi lililosimamisha mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi bado lipo na lina uwezo mkubwa zaidi kuliko miaka 32 iliyopita.

Waziri Nduhungirehe aonya wanaotaka kuvuruga Usalama wa Rwanda kwamba Jeshi lililositisha Mauaji ya kimbari bado lipo

Katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka ya 32 ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi, yaliyofanyika katika Kituo cha Ukumbusho cha Nyanza ya Kicukiro tarehe 11 Aprili 2026, Waziri Nduhungirehe alieleza kuwa wahusika wa mauaji hayo waliunda kundi la FDLR linaloendesha shughuli zake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waziri Nduhungirehe amesema ni jambo lisiloeleweka kuona kwamba, miaka 32 baada ya kusimamishwa kwa mauaji ya kimbari, FDLR bado iko karibu na mpaka wa Rwanda na inaungwa mkono na serikali ya DRC inayoongozwa na Rais Félix Tshisekedi, ambaye amesema ana mpango wa kushambulia Kigali.

Alieleza kuwa dalili zinazoashiria uwezekano wa mauaji ya kimbari nchini DRC bado zipo, akibainisha kuwa lugha ya chuki inayowalenga Watutsi inaendelea kusambazwa, ikiwemo kuwaita “inyenzi” na majina mengine ya kuwadharau, kama ilivyokuwa katika miaka ya 1990.

Waziri Nduhungirehe alisema kuwa licha ya dhuluma zote zinazoifanyiwa Rwanda, nchi hiyo itaendelea kukabiliana nazo huku ikilinda usalama wa mipaka yake na raia wake ili wasitishwe na kundi la kigaidi pamoja na washirika wake.

Aliwahakikishia Wanyarwanda kuwa jeshi la Rwanda linaendelea kulinda usalama wa nchi kikamilifu, na kwamba wanaotaka kuivuruga watashindwa kama ilivyokuwa miaka 32 iliyopita walipositisha mauaji ya kimbari na kuikomboa nchi.

Alisema, “Jeshi lililositisha mauaji ya kimbari bado lipo. Halijatoweka, na sasa lina uwezo mkubwa zaidi kuliko wakati huo. Katika ukanda huu au kwingineko, yeyote anayefikiri anaweza kurudisha giza la zamani anajidanganya. Inkotanyi bado ni zile zile.”

Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi yalitekelezwa kuanzia tarehe 7 Aprili hadi 4 Julai 1994, ambapo zaidi ya watu milioni moja waliuawa ndani ya siku 100 tu.

Bagabo John