Jeshi la Rwanda kupitia tuvuti ya X , limetangaza kwamba leo tarehe 23 Mei 2025, Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Daniel Chapo ameongoza hafla ya kufuzu kwa wanajeshi 525.
Leo, Rais wa Msumbiji ambae pia ndie Amirijeshi mkuu jeshi la Msumbiji (FADM), Mheshimiwa Daniel Chapo, ameongoza hafla ya kufuzu kwa wanajeshi 525 wa Msumbiji katika kozi ya juu ya askari wa nchi kavu, waliopewa mafunzo na wakufunzi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda. (RDF)

Sherehe ya kuhitimu imefanyika katika Kituo cha Mafunzo cha Nacala katika Mkoa wa Nampula baada ya kukamilisha mafunzo hayo yaliyo dumu kwa miezi sita .

Bagabo John
