Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema ana matarajio ya kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo, akidai anaweza kupata hadi asilimia 80 ya kura iwapo hakutakuwa na udanganyifu wowote katika mchakato wa uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura, Museveni amesema hana hofu ya kushindwa, akisisitiza kuwa ana imani na uungwaji mkono wa wananchi kutokana na rekodi ya utendaji wa serikali yake.

Ameonekana kupuuzia kabisa uwezekano wa kupoteza uchaguzi huo dhidi ya mpinzani wake mkuu, mwanamuziki aliyebadili mwelekeo na kuingia kwenye siasa, Bobi Wine, akisema hana wasiwasi wowote kuhusu ushindani huo.
Bagabo John
