Leo tarehe 24 Feburary 2026 Katika Tarafa ya Mahama, Wilaya ya Kirehe, Ofisi ya Taifa ya Upelelezi (RIB) imefanya kampeni ya uhamasishaji inayolenga kuhimiza kila mtu kushiriki katika kuzuia na kupambana na uhalifu wa biashara haramu ya binadamu.
Katika kampeni hizo, Naibu Mkuu wa Wilaya anayehusika na masuala ya ustawi wa jamii, MUKANDAYISENGA Janviere
ameungana na wananchi katika kampeni ya kupambana na uhalifu wa biashara haramu ya binadamu iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Upelelezi (RIB)

Naibu Mkuu wa Wilaya anaye husika na ustawi wa jamii Mukandayisenga Janviere
Amewahimiza wananchi kutoa taarifa kwa wakati ili kuzuia uhalifu huo mapema.

Katika kampeni ya uhamasishaji dhidi ya uhalifu wa biashara haramu ya binadamu
Ofisi ya Taifa ya Upelelezi (RIB)
Imefafanua maana ya biashara haramu ya binadamu, mbinu zinazotumiwa, wahusika wake, adhabu zinazotolewa pamoja na wajibu wa kila mmoja katika kuzuia uhalifu huo.

Bagabo John
