•     

Vigogo sita wa Chama CCM tayari wamechukua fomu kuwania nafasi ya Spika wa Bunge

Taarifa zinaonyesha kuwa vigogo sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tayari wamechukua fomu kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nafasi ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa mwaka huu.

Wanaotajwa kuchukua fomu ni:

1. Dkt. Tulia Ackson – Spika anayemaliza muda wake.

2. Prof. Palamagamba Kabudi – Mwanasheria hodari na mbunge wa muda mrefu.

3. William Lukuvi – Kiongozi mwenye uzoefu mpana serikalini.

4. George Simbachawene – Mbunge na waziri mwenye ushawishi ndani ya chama.

5. Zungu – Mwanasiasa mkongwe kutoka Dar es Salaam.

6. Najma Murtaza Giga – Mwenyekiti wa muda mrefu wa Bunge, anayejulikana kwa nidhamu na uthabiti.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani vya chama, mchuano wa safari hii umeelezewa kama “mechi ya fainali”, kutokana na uzito wa kisiasa na kiutendaji wa kila mgombea.

Mitandaoni, mjadala tayari umeanza kushika kasi — baadhi ya wananchi wakimtaka Dkt. Tulia aendelee kutokana na uzoefu wake, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa damu mpya katika uongozi wa chombo hicho muhimu cha dola.

Bagabo John 