Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) wametoa barua rasmi wakielezea whasiwasi mkubwa kuhusu kutoweka kwa Balozi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Humphrey Polepole, ambaye hajulikani alipo tangu Oktoba 6.
Barua hiyo iliyosainiwa na Barry Andrews, Robert Biedroń, Udo Bullmann, Michael Gahler, Erik Marquardt na David McAllister, imelaani kile walichoeleza kuwa ni mfululizo wa vitendo vya utekaji, mateso na vitisho vinavyowalenga wanasiasa wa upinzani, waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania.
Wabunge hao wameitaka Serikali ya Tanzania kuwaachia mara moja watu wote waliotekwa, kuhakikisha usalama wao, kuchunguza matukio hayo na kuwawajibisha wahusika. Pia wametaka hatua za kukomesha utamaduni wa kutowajibika na kuimarishwa kwa uhuru wa kujieleza na kukusanyika.

Aidha, barua hiyo imeitaka Umoja wa Ulaya (EU) kufuatilia kwa karibu hali hiyo, kutumia diplomasia kuihimiza Tanzania kuchukua hatua, na kuunga mkono taasisi za kiraia zinazotetea haki za binadamu.
Kutoweka kwa Polepole kumezua taharuki kimataifa huku mashirika ya haki za binadamu na serikali za kigeni zikitaka uwazi na uwajibikaji, hususan kuelekea uchaguzi wa Oktoba 29 nchini Tanzania.
Bagabo John
