•     

Wakatoliki wapeleka Malalamiko yao Ubalozi wa Vatican

Kundi la waumini wa Kanisa Katoliki linalokadiriwa kufikia watu 100, leo Januari 5, 2026, limefika katika Ubalozi wa Vatican nchini Tanzania kuwasilisha barua rasmi ya malalamiko dhidi ya viongozi wawili waandamizi wa kanisa hilo.

Malalamiko hayo yanawalenga Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kutoridhishwa kwa baadhi ya waumini na maudhui ya mahubiri yaliyotolewa na Kardinali Ruwa’ichi wakati wa Misa ya Krismasi, Desemba 25, 2025. Waumini hao, wanadai kuwa lugha iliyotumika madhabahuni ilikuwa na mwelekeo wa ukali, vitisho, na hukumu badala ya kutoa faraja na mafundisho ya upendo.

Wanalalamika kuwa mimbari imetumika kushambulia waumini waliokuwa wamewasilisha hoja zao kwa Balozi wa Vatican hapo awali, jambo ambalo wanadai linakiuka misingi ya kichungaji na heshima ya waumini ndani ya kanisa.

Malalamiko hayo yanamhusisha pia Padri Dkt. Charles Kitima, ambaye anadaiwa na kundi hilo la waumini kukiuka misingi ya utumishi wake kwa kujiingiza katika masuala ya kisiasa.

Bagabo John 