Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Rwanda wameanza Mashindano ya kusoma na kuandika vitabu Wanafunzi kutoka vyuo vikuu 23 vya Rwanda wameanzisha Mashindano ya kusoma na kuandika vitabu ikiwa lengo la kuwafunza sanaa ya uandishi wa vitabu vinavyohusu mada mbalimbali ikiwemo historia ya Rwanda na kujifunza maadili yanayowatambulisha wanyarwanda.
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu 23 vya Rwanda wameanzisha Mashindano ya kusoma na kuandika vitabu ikiwa lengo la kuwafunza sanaa ya uandishi wa vitabu vinavyohusu mada mbalimbali ikiwemo historia ya Rwanda na kujifunza maadili yanayowatambulisha wanyarwanda.
Ni shindano lililozinduliwa Machi 3, 2025, lililofanyika kwa mara ya tatu, ambapo linalenga kuhamasisha vijana wanaosoma katika vyuo vikuu mbalimbali vya Rwanda, kusoma na kuandika, hasa historia ya Rwanda.
Mkuu wa Chama cha Waandishi nchini Rwanda, Hategekimana Richard amesema kuwa shindano hili ni njia ya kukuza utamaduni wa kusoma na kuandika, historia na utamaduni wa Rwanda vitapewa kipaumbele.

Mkuu wa Chama cha Waandishi nchini Rwanda, Hategekimana Richard
Alisema, "Lengo la kwanza ni kutoa mafunzo kwa watoto wa Rwanda ili kuimarisha maadili ya Rwanda. Tumechagua vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini pia tumetayarisha na kuandika kwa lugha zingine ili wageni wanaosoma hapa waweze kushiriki na kujifunza juu ya maadili haya."
Aliendelea kusema, "Vijana lazima wawe na uwezo wa kuandika habari za Rwanda kwa sababu imepata mafanikio makubwa, wageni wanatuzidi kuandika histolia ya Nchi yetu, sanyingine unakuta wamepotosha ukweri kuhusu Rwanda.

Washindi wa shindano hili katika ngazi ya kitaifa watalipwa fedha zitakazowasaidia kulipia karo ya shule, au kuanzisha miradi itakayowasaidia kujiendeleza na kadhalika.
Wakati huu takriban wanafunzi 2,000 kutoka vyuo vikuu 23 nchini walishiriki, walifanya mtihani wa kusoma na kuandika kwa Kinyarwanda, washindi watatunukiwa Machi 27, 2025.
Bagabo John
