•     

Green Party imezindua rasmi mfumo wa kuhifadhi taarifa za wanachama

Chama cha Democratic Green Party of Rwanda chazindua rasmi mfumo wa kisasa wa kuhifadhi taarifa za wanachama kwa njia ya mtandao (Online Membership Database), hatua inayolenga kuboresha usimamizi wa wanachama na kuimarisha mawasiliano ndani ya chama hicho.

Mkutano huo uliwakutanisha viongozi wa chama, makamishna pamoja na wanachama mbalimbali kwa lengo la kujadili mwelekeo wa chama na shughuli muhimu zilizopangwa kwa miaka ijayo.

Akifungua mkutano huo, Rais wa chama cha Democratic Green Party of Rwanda, Seneta Dkt Frank Habineza, aliwakaribisha washiriki na kueleza ajenda kuu zilizokuwa kwenye ratiba ya majadiliano. Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni mafunzo yanayohusiana na uhifadhi wa mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo yanaendelea kuwa moja ya nguzo kuu za chama hicho.

Mkutano huo pia ulitumika kama fursa ya kuwatambulisha makamishna wapya pamoja na wanachama wapya waliojiunga na chama hicho kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Moja ya mambo yaliyopewa uzito katika mkutano huo ni uzinduzi rasmi wa mfumo wa kisasa wa kuhifadhi taarifa za wanachama kwa njia ya mtandao (online membership database).

Dkt, Habineza alisema kuwa mfumo huo mpya wa kidijitali utasaidia kuboresha ushirikiano na mawasiliano kati ya vyombo vya chama, pamoja na kurahisisha usimamizi wa wanachama.

         Seneta Dkt Frank Habineza 

Katika mkutano huo pia, viongozi wa chama waliwasilisha mpango mpya wa muda mrefu wa maendeleo (Strategic Plan) pamoja na mkakati mpya wa mawasiliano (Communication Strategy), ambayo yataongoza mwelekeo na utendaji wa Democratic Green Party of Rwanda katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Bagabo John 