Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) limefanya maboresho ya Liturujia katika baadhi ya vipengele ikiwemo kipengele cha matangazo ambapo awali viongozi waliruhusiwa kutoa neno na sasa haitakuwa hivyo tena.
Kama Misa imehudhuriwa na Rais, Waziri, Mbunge au kiongozi mwingine yeyote, Padre/Askofu anayeendesha ibada atatambua uwepo wake bila kumpa nafasi yoyote ya kuongea.
Ikiwa kiongozi ana sadaka au neno la shukrani basi Katekista, Padre au Askofu atatoa shukrani hizo kwa niaba ya kiongozi husika.

Mabadiliko hayo yametoa katazo kwa kipengele hicho na kuanzia sasa wageni ikiwemo viongozi wa kiserikali hawatoruhusiwa kuzungumza ndani ya Kanisa Katoliki
Hakutakuwa na hotuba za kupongezana, isipokuwa tu Mwadhimishaji (Paroko, Padri kama ni tukio la kiparokia, Askofu wa jimbo kama ni tukio la jimbo, Rais wa TEC kama ni tukio la kitaifa) atatambua kwa ufupi uwepo wa wageni wa kidini, kiserikali, kijamii na waalikwa wote bila kuwapa nafasi ya kuongea, kutoa hotuba wala kusalimia"-imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Bagabo John
