Msemaji wa Polisi wa Rwanda (ACP) Boniface Rutikanga alisema kuwa matumizi ya dawa za kulevya yanaendelea kuonekana katika makundi mbalimbali ya watu, huku baadhi ya watumiaji wakiwa na hali ya kiafya inayohitaji kupatiwa matibabu.
Tarehe 26 Juni kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi mabaya ya dawa za kulevya na biashara haramu lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi kuacha kutumia dawa hizo na kuwasaidia kujikwamua na baadhi ya madhara yake kwa afya ya binadamu.
Ujumbe uliotolewa na Polisi wa Kitaifa wa Rwanda kwa ushirikiano na Tume ya Afya ya Rwanda (RBC) uliangazia athari za dawa za kulevya na jukumu la familia katika kufanya kazi pamoja ili kukabiliana na utumiaji wa dawa za kulevya, haswa miongoni mwa vijana
Katika kipindi cha miezi 6, kuanzia Januari hadi nusu ya kwanza ya Juni 2025, watu 778 walikamatwa kwa kusafirisha, kusambaza na kutumia dawa za kulevya, ambapo zaidi ya 87.5% walikuwa chini ya umri wa miaka 40, ikionyesha kuwa watumiaji wengi ni vijana.

Msemaji wa Polisi ACP Boniface Rutikanga Alisema: “Kumiliki na kusambaza dawa za kulevya ni kosa linalopaswa kuadhibiwa kisheria, pamoja na ukweli kwamba mtumiaji amenunua, na kwa sababu ni uraibu, inamtaka wakati wowote anapozihitaji, apate, akikosa fedha atafute mbinu za kuiba ili kuzipata, jambo ambalo linasababisha uhalifu mwingine unaofuata ikiwa ni pamoja na kushambulia na kuwapiga, tabia mbaya, migogoro ya kifamilia na mengineyo.”
Kifungu cha 263 cha Sheria ya Makosa ya Jinai na Adhabu za Jumla kinasema mtu yeyote atakayekamatwa akila, kunywa, kumeza, kuvuta au kwa njia yoyote ile akimeza dawa ndogo au mchanganyiko wa dawa zinazotumika kwa njia hiyo hiyo, anatenda kosa.

Iwapo atatiwa hatiani na mahakama, ataadhibiwa kwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja 1 lakini kisichozidi miaka miwili 2
Bagabo John
