Mke wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga, amekanusha vikali barua inayosambaa mitandaoni ikidai amejiuzulu.
Amesema barua hiyo haina ukweli wowote na si yeye aliyeiandika, akibainisha kuwa kwa sasa familia ipo kwenye maombolezo ya kumpoteza mume wake, hivyo hana sababu wala nguvu za kuandika barua hiyo.
Aidha, Dkt. Mganga ameeleza kuwa walioandika na kusambaza barua hiyo wana nia ovu dhidi ya familia yao, na ameiomba serikali kuwachukulia hatua wote waliohusika kuandaa na kusambaza taarifa hiyo ya uongo.

Bagabo John
