•     

Rais Kagame Ateuliwa Kuongoza Tume ya Umoja wa Mataifa Inayosimamia Akili Mnemba

Rais Paul Kagame ameteuliwa kuwa Mwenyekiti Mkuu wa Tume mpya ya Umoja wa Mataifa inayosimamia kuendeleza matumizi ya Akili Mnemba (AI) duniani, AI for Good Global Commission.

Rais Kagame atashirikiana katika jukumu hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya teknolojia ya Salesforce, Marc Benioff, huku Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano (ITU), Doreen Bogdan-Martin, akihudumu kama Makamu Mwenyekiti.

Lengo kuu la kuundwa kwa tume hiyo ni kuhakikisha Akili Mnemba  (AI) inachangia kupunguza pengo la kiteknolojia kati ya mataifa, na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea.

Tume hiyo imeanza kazi ikiwa na nguvu kubwa, ikiwajumuisha zaidi ya viongozi 40 kutoka sekta mbalimbali.

Miongoni mwa wanachama wake ni viongozi wa kampuni kubwa za teknolojia duniani, akiwemo Jensen Huang wa Nvidia, Andy Jassy wa Amazon, Brad Smith wa Microsoft, pamoja na viongozi wa kampuni zinazojihusisha na Akili Bandia (AI) kama Anthropic na Cohere.

Pia tume hiyo inawajumuisha viongozi kutoka Accenture na Reliance Industries, Marais wa Estonia na Iceland, mawaziri kutoka serikali za Singapore na Nigeria, pamoja na viongozi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara (UN Trade) na Umoja wa Afrika.

Bagabo John 